
Kupitia azimio lililowasilishwa na Ufaransa, Baraza limeamua kwamba MONUSCO itaendelea kuwa na idadi ya juu iliyoidhinishwa ya wanajeshi 11,500, waangalizi wa kijeshi na maafisa wa makao makuu 600, askari polisi 443, na wafanyakazi1,270 wa vitengo vya polisi vilivyoundwa.
Pia linaamua kwamba vipaumbele vya kimkakati vya MONUSCO ni kuchangia: ulinzi wa raia katika eneo lake la upelekwaji; utekelezaji wa malengo yaliyowekwa na azimio 2773 (2025); na utulivu pamoja na uimarishaji wa taasisi za kitaifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Usitishaji mapigano
Zaidi ya hayo, Baraza linaidhinisha MONUSCO kusaidia utekelezaji wa sitisho la kudumu la mapigano kwa mujibu wa azimio 2773 (2025).
Baraza la Usalama linakumbusha kwamba eneo la operesheni la MONUSCO limewekewa mipaka katika majimno ya Kivu Kaskazini na Ituri. Pia kumekuwepo kusitishwa kwa muda kwa mpango uliokubaliwa wa kujiondoa kwa MONUSCO, kutokana na mabadiliko ya hali ya usalama katika uwanja wa operesheni.