Fletcher ameongeza kuwa pamoja na ukarimu huo, mageuzi yako katika kiini cha kazi inayotarajiwa kufanywa kati ya Marekani, OCHA na mfumo mzima wa kibinadamu.
Amebainisha kuwa walipa kodi wa Marekani wanastahili kujua jinsi msaada wao unavyotumika, na kwamba OCHA ingeonesha namna kila dola inavyotoa matokeo halisi ya kuokoa maisha.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. WFP inatoa chakula cha dharura kwa familia zinazotoroka vurugu huko Uvira, kuhakikisha hakuna mtu anayefa njaa wakati wa mgogoro
Urasimu unapunguzwa
Amefafanua kuwa kwa kuunga mkono fedha za nchi, Marekani pia inaweka kura muhimu na ya kutia moyo ya imani na ujasiri katika Mpango wa Mageuzi ya Kibinadamu, ambao kupitia kwake hatua za kibinadamu zinafanywa kuwa za haraka zaidi, zenye ufanisi zaidi na zilizo karibu zaidi na watu walioko mstari wa mbele wa dharura.
Amesema kuwa urasimu unapunguzwa, urudufu wa kazi unaondolewa, na vipaumbele vinawekwa kwa umakini huku juhudi zikilenga kuokoa maisha ya watu milioni 87 mwaka 2026.
Kwa kumalizia, Fletcher amesema kuwa kwa muda mrefu Marekani imekuwa nguvu kuu ya kibinadamu duniani, na kwamba mamia ya mamilioni ya watu wako hai leo kutokana na ukarimu wa Marekani.
Amesema mamilioni zaidi ya watu watanusurika mwaka 2026 kutokana na uwekezaji huo wa kihistoria katika ubinadamu.
Programu ya Chakula Duniani yasambaza misaada nchini Afghanistan
Guterres akaribisha dola bilioni 2 toka Marekani
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amekaribisha kwa dhati ahadi mpya kubwa ya kibinadamu iliyotolewa leo na Marekani, ikitangaza mchango wa awali wa dola bilioni 2 kusaidia operesheni za kuokoa maisha zinazoongozwa na Umoja wa Mataifa kote duniani.
Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake jijini New York Katibu Mkuu amesema mchango huo utaimarisha kwa kiasi kikubwa uwezo wa Umoja wa Mataifa kuokoa maisha, kuwafikia walio hatarini zaidi, na kupunguza mateso ya binadamu wakati mahitaji ya kibinadamu yanaendelea kuongezeka katika maeneo mbalimbali ya dunia.
“Taarifa hiyo imesema mchango huu utaongeza uwezo wetu wa kuokoa maisha, kutoa misaada kwa walio hatarini zaidi na kupunguza mateso ya binadamu,” ikibainisha mzigo unaoongezeka unaowakabili wahudumu wa misaada ya kibinadamu kutokana na migogoro, majanga yanayohusiana na mabadiliko ya tabianchi, pamoja na misukosuko ya kiuchumi inayoathiri mamilioni ya watu.
Timu za BLDA zikiandaa mahema kwa ajili ya watu waliokimbia makazi yao Gaza
Kila dola ni muhimu
Katibu Mkuu amesisitiza kuwa matumizi bora ya fedha hizo yatapewa kipaumbele cha juu. “Kila dola ni muhimu na tumejizatiti kutumia msaada huu kikamilifu ili kutoa matokeo halisi kwa watu wanaohitaji msaada wa dharura,” taarifa hiyo imeongeza.
Wakati mahitaji ya kibinadamu yakifikia viwango vya juu zaidi duniani, Katibu Mkuu pia amezitaka serikali na wafadhili wengine kuongeza mchango wao. Ameitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza juhudi zake kukabiliana na kile ambacho Umoja wa Mataifa umekuwa ukikielezea mara kwa mara kama mgogoro wa kibinadamu unaozidi kuongezeka duniani.
Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Stéphane Dujarric, katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.