
Jarida maarufu dunia la Fobes limemtaja mwanamuziki wa Pop, Beyonce kuwa rasmi ni bilionea, hatua iliyopelekea kuingia top 5 ya wanamuziki matajiri zaidi duniani.
Beyonce mwenye umri wa miaka 44, anaungana na wanamuziki wengine katika orodha hiyo akiwemo mumewe rapa, Jay-Z, Tylor Swift, Bruce Springteen, na Rihanna, ambapo Beyonce sasa anatajwa kufikia utajiri wa zaidi ya dola bilioni 1 sawa na za sh2.4 trilioni.
Jarida hilo limeeleza kuwa sababu ya mafanikio hayo ni kutokana na mauzo ya ziara yake ya Rennaissence tamasha lililoingiza pesa nyingi zaidi duniani mwaka 2025, mauzo ya albamu yake bora ya Country Cowboy Carter (2024), Pafomansi yake usiku wa Christmas Day Halftime shoo ambayo ipo chini ya NFL, Ushirikiano wake na Levis, biashara pamoja na dili nyingine.
Beyoncé alianza kujenga himaya yake imara ya kibiashara rasmi mwaka 2010, alipoanzisha Parkwood Entertainment iliyoleta udhibiti wa kazi yake. Kampuni hiyo inasimamia kazi zake ikiwa ni pamoja na muziki, filamu za uhalisi (Reality) na matamasha yake ya muziki.
“Nilipoamua kujisimamia, ilikuwa muhimu kwamba nisiende kwenye kampuni kubwa ya usimamizi, nilihisi kama nataka kufuata nyayo za Madonna na kuwa mtu mwenye nguvu na himaya yangu mwenyewe na kuonyesha wanawake wengine unapofikia hatua hii ya kazi yako sio lazima uende kusaini na mtu mwingine na kushiriki pesa zako na mafanikio yako unafanya mwenyewe.” alisema Beyonce wakati wa mahojiano yake 2013.
Hata hivyo, ukiachilia mbali Queen Bey kupanua himaya yake ya biashara katika sekta nyingine ikiwa ni pamoja na brandi ya utunzaji wa nywele (Cécred), lebo ya whisky (SirDavis), unaambiwa utajiri wake kwa kiasi kikubwa unatokana na muziki wake, akifanikiwa kudhibiti haki za kupata mapato yake makubwa kutoka kwa orodha kubwa ya mapato yake ya kimataifa.
Ziara yake ya Cowboy Carter ambayo inatajwa kuingiza mtonyo mrefu zaidi 2025 ilisimamiwa na zaidi ya wahudumu 350, vifaa vyenye thamani ya lori 100, na ndege nane za mizigo kuihamisha kutoka jiji hadi jiji.
Kulingana na makadilio ya Forbes kwa ujumla, Cowboy Carter Tour ilipata zaidi ya dola 400 milioni katika mauzo ya viingilio kwenye shoo zake, na kwa sababu kampuni yake ya Parkwood ndio ilizalisha yote, Beyoncé aliweza kupata kiasi cha juu cha faida.
Kwa kuchanganya alichofanya utalii na mapato kutoka kwa orodha yake ya muziki na mikataba ya ufadhili mwaka huu, Forbes inakadiria kuwa aliingiza kiasi cha dola milioni 148 mwaka 2025, na hivyo kumfanya kuwa mwanamuziki wa tatu anayelipwa zaidi duniani.
Kiwango hiki cha mafanikio ya kifedha kwa Beyonce kimeongezeka polepole kwa miaka mingi, haswa baada ya kutengana na kundi la Destiny’s Child mwanzoni mwa miaka ya 2000 na kuacha kusimamiwa na baba yake mzee Mathew Knowles mwaka 2010.
Pia alipata njia mpya za kuorodhesha muziki wake, pamoja na albamu ya kushitukiza aliyoipa jina la Beyoncé iliyotoka 2013, Home Coming ya Coachella 2018 ambayo alikuwa msanii kinara akiwavutia watazamaji 458,000 YouTube na kuibua filamu ya hali ya juu ya Netflix ambayo alipokea takriban dola 60.