Marekani na washirika wa Ulaya wa Ikulu ya White House wameshindwa katika vita laini dhidi ya Iran ya Kiislamu, licha ya kutumia kiwango kikubwa cha fedha na mashirika ya propaganda na kuenea kwa uwongo.
Vita laini (soft war) vya Marekani na Magharibi dhidi ya Iran vimekuwa vikifeli na kushindwa kutokana na mshikamano wa kitaifa, uongozi wenye busara, kufeli vyombo vya ujasusi vya adui, na radiamali na majibu makini ya umma. Adui wa Jamhuri ya Kislamu ameshindwa kufikia malengo yake maovu hadi sasa, kutokana na makosa ya mahesabu na kupuuza uwezo wa kitamaduni na kijamii wa Iran.
Vituo vya kisiasa na propaganda vya Marekani na Magharibi vimefanya makosa mara kwa mara katika kuchambua hali ya Iran na vimepuuza uwezo wa kitamaduni, kijamii, na kisiasa wa nchi hii. Maafisa wa serikali ya Marekani walidhani kwamba wangeweza kuwatenganisha watu wa Iran na serikali kupitia mashinikizo ya vyombo vya habari na vikwazo vya kiuchumi, lakini lengo hili halijawahi kufikiwa.

Katika nyakati muhimu, ikiwa ni pamoja na kipindi cha vita vya mseto vya hivi karibuni, watu wa Iran walizuia njama za adui kwa kuhudhuria ipavyo uwanjani. Majiibu ya wananchi yalizuia vita laini kuenea nchini, na adui alishindwa kuibua mgogoro mkubwa wa kijamii ndani ya nchi. Kwa upande mwingine, miongozo ya busara ya Kiongozi wa Mapinduzi tya Kiislamu katika kujenga matumaini na kuimarisha ari ya kitaifa daima imekuwa na mchango muhimu katika kushindwa vita laini, na usimamizi wa busara umemzuia adui kutumia mapengo ya kijamii.
Uwezo wa kiintelijensia na kijasusi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia umeweza kuzuia mipango mingi ya adui na kuzuia kufikiwa kwa malengo mabaya ya Magharibi dhidi ya Iran. Sambamba na hayo, Iran imeweza kujibu vitisho katika kipindi kifupi na kuonyesha kwamba uwezo wake wa kiulinzi na kijeshi unazidi sana mawazo ya adui. Uwezo huo wa kijeshi ni nguzo muhimu katika kukabiliana na vita laini.
Akihutubia mahfali ya kumbukumbu ya kuzaliwa Imam Ali bin Abi Twalib (AS) na hauli ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, iliyohudhuriwa na familia za mashahidi wa vita vya siku 12, Ayatullah Khamenei alisisitiza udharura wa kuwa macho na makini na kuimarisha umoja wa kitaifa katika kukabiliana na vita laini na kusema: Vita hivi ambavyo msingi wake ni “udanganyifu, uongo, tuhuma na uvumi” ni vita vilevile viliyoanzishwa na maadui wa serikali ya Imam Ali bin Abi Twalib baada ya kushindwa kijeshi ili kuzuia kutimizwa malengo yake.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kwamba lengo la adui katika vita laini ni kuwakatisha tamaa wananchi na kuibua hali ya shaka katika taifa na kusisitiza kwamba: Kama ambavyo katika zama za Amirul Muuminina, walijaribu kuwafanya watu wakate tamaa kwa kueneza uvumi na uongo, hii leo mbinu hiyo hiyo pia inatumika, lakini taifa la Iran limeonyesha kwamba katika nyanja ngumu na popote pale msaada wake unapohitajika, linasimama imara na kumkatisha tamaa adui.

Vita laini vya adui dhidi ya Iran vinategemea zaidi zana za vyombo vya habari, masuala ya kitamaduni, kijamii na uharibifu ili kulenga imani, utambulisho na mshikamano wa kitaifa. Uzoefu wa miaka iliyopita umeonyesha kwamba, wakati wowote adui anapoingia uwanjani na propaganda chafu za vita vya kisaikolojia, mahudhurio ya haraka ya wananchi na usimamiaji mzuri wa migogoro nchini hupelekea kushindwa kwa mipango yake.
Kwa hivyo, nguvu laini ya Iran, ambayo imejikita katika utamaduni, imani ya kidini na mshikamano wa kijamii, imekuwa kikwazo muhimu zaidi dhidi ya vita laini vya adui.