#HABARI: Waziri wa Katiba na Sheria, Juma Homera, ameliagiza Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, kupitia Dawati la Jinsia na Watoto, kumsaka na kumkamata Daniel Simbaulanga, mkazi wa Morogoro, kwa tuhuma za kumtelekeza na kumnyanyasa mkewe, Victoria Zackaria, pamoja na mtoto mchanga mwenye umri wa miezi mitano.

Agizo hilo limetolewa leo Jumatatu, Januari 5, 2026, wakati wa Kliniki ya Huduma za Msaada wa Kisheria mkoani Morogoro, baada ya Victoria kujitokeza mbele ya Waziri na kueleza masaibu mazito anayopitia.

Kwa uchungu, Victoria alieleza kuwa unyanyasaji huo ulianza wiki tatu tu baada ya yeye kufanyiwa upasuaji (operation) wa kujifungua.

Amedai kuwa mumewe hakuwahi kutoa msaada wowote wa kifedha tangu akiwa hospitali na badala yake alimfukuza nyumbani huku akimshutumu kuwa mtoto huyo si wake.

Victoria ameongeza kuwa mumewe huyo amekuwa akimtumia ujumbe wa kejeli kwenye simu akimkataza kukanyaga katika nyumba yao, huku akijivunia kuishi na mwanamke mwingine.

‎Powered by #MCHEZOSUPA

‎‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *