#HABARI: Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kuhakikisha inakamilisha kwa asilimia 100 maabara ya Phizikia ya Shule ya Sekondari Igalamya Kata ya Usule ili wanafunzi waweze kujifunza masomo ya sayansi kwa vitendo zaidi kuliko nadharia hali itakayosaidia utekelezaji wa juhudi za Serikali kuhakikisha wanafunzi wanafaulu masomo ya sayansi kwa kiwango cha juu.
Mkuu huyo wa mkoa ametoa agizo hilo wakati akikagua ujenzi wa maabara hizo tatu za Phizikia, Kemia na Bioliojia huku akieleza kuwa wakati umefika watumisi wa Serikali hasa wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha wanatumia vyanzo vya mapato kuibua miradi ya vipaumbele vya wananchi ili kupunguza malalamiko.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.