#Habari: Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Kusini, limeteketeza bidhaa mbalimbali zisizofaa kwa matumzi ya binadamu ikiwemo nguo za ndani za mitumba, vipodozi na vinywaji vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni ishirini.
Akizungumza mara baada ya uteketezaji wa bidhaa hizo Meneja wa TBS Kanda ya Kusini, Bw. Abel Mwakasonda, amesema shirika hilo litaendelea kutoa elimu ili wananchi waache kuvaa kungo za ndani za mitumba na bidhaa zilizokwisha muda wake.
Vilevile pia Bw. Abel amebainisha malengo ya Serikali ya kuzuia uvaaji wa nguo za ndani za mitumba na bidhaa zilizokwisha muda wake ni kulinda afya za wananchi wake ikiwa ni pamoja na kuzuia kupata magonjwa ya ngozi.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Mtwara Richard Mwalingo amewataka TBS kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kutambua athari za vyakula vilivyokwisha muda wake lakini pia vipodozi visivyofaa.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.