Serikali ipo mbioni kuandaa Sera ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria itakayoweka misingi ya kuboresha na kuimarisha upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi wote.

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt Juma Zuberi Homera akizinduzi kliniki ya huduma za msaada wa kisheria zinazotolewa bure mkoani Singida amesema sera hiyo itajikita katika maeneo mbalimbali.

Ameyataja maneno hayo kiwa ni pamoja na utatuzi wa migogoro, kuanzisha na kuendesha madawati ya msaada wa kisheria katika ngazi za halmashauri na kuimarisha matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Amesema lengo la.Serikali ni kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma za msaada wa kisheria na kuzifikia halmashauri zote nchini.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Zainab Katimba, amesema wizara hiyo imeanzisha kituo cha huduma kwa mteja kinachopatikana kupitia namba 0262160360, kinachosaidia kuongeza uelewa wa jamii kuhusu namna ya kuripoti na kushughulikia matukio ya ukatili wa kijinsia.

Meneja wa Usajili wa Vizazi, Vifo, Ndoa na Talaka wa RITA, Patricia Mpuya amesema wamepokea maombi 122,000 ya vyeti vya kuzaliwa kuanzia Desemba 15 mwaka jana na 110,000 sawa na asilimia 91 yamefanyiwa kazi na wananchi kupokea vyeti vyao ndani ya saa 48 za kazi.

#StarTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *