Katika mitaa ya makazi ya wakimbizi wa ndani ya Nuseirat, akipita na Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kwa Eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel, Moreira da Silva mesisitiza kuwa urejeshaji wa maisha ya watu Gaza hauwezi kusubiri hasa linapokuja suala la nishati ya umeme.

“Umeme ni nguzo muhimu inayowezesha kila kitu kingine kufanya kazi afya, elimu, kaya. Jamii nzima na uchumi hutegemea upatikanaji wa umeme wa uhakika na wa gahrama wanayoimudu. Kwa bahati mbaya, leo Gaza haina kabisa upatikanaji wa umeme.”

Kutoka kambini, msafara huo wa Umoja wa Mataifa uliendelea hadi katika kituo cha kuzalisha umeme cha Gaza, ambacho kwa sasa hakifanyi kazi ipasavyo baada ya uharibifu Mkubwa uliosababishwa na vita na uhaba wa mafuta.

Jorge Moreira da Silva, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkurugenzi wa UNOPS, anatembelea ukanda wa Gaza, akisimama karibu na kituo cha uzalishaji wa umeme na magari ya Umoja wa Mataifa yameegeshwa nje.

Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kwa Eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel, Moreira da Silva anatembelea ukanda wa Gaza kutathmini hali ya kibinadamu katika kituo cha umeme.

Akiwa ndani ya kituo hicho, Moreira da Silva alionya kuwa bila ukarabati wa haraka, hata huduma za msingi zitaendelea kusimama.

“Ni muhimu sana kwamba tunaposubiri ujenzi mpya mkubwa wa baadaye, tusipoteze hata dakika moja. Tunahitaji msaada wa haraka kurekebisha kituo cha umeme na vipuri vinavyohitajika viruhusiwe kuingia, na kazi ianze mara moja.”

Amesema kurejesha umeme hakuhusu kituo cha uzalishaji pekee, bali mfumo mzima kuanzia hifadhi ya mafuta hadi njia za usambazaji.

“Kwa neno moja, ni wakati wa kuchukua hatua. Hapa hatuzungumzii mabilioni ya dola. Tunahitaji dola milioni kumi mara moja ili kurejesha umeme Gaza.”

Maafisa hao wa Umoja wa Mataifa walipoondoka katika eneo hilo, ujumbe wao ulikuwa bayana bila umeme, urejeshaji wa maisha Gaza hauwezi kuanza na bila msaada wa haraka wa jumuiya ya kimataifa, giza totoro litaendelea kuwa sehemu ya maisha ya kila siku hapa katika makazi ya Nuseirat.

Kwa sasa UNOPS na mashirika mengine ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa wanafanya kila liwezekanalo kutoa mahitaji ya msingi kwa wakimbizi wa ndani waNuseirat ambao ili kuishi wanategemea msaada wa kibinadamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *