Gholamhossein Darzi, Naibu Mwaklishi wa Kudumu wa Iran Umoja wa Mataifa ameikosoa vikali Marekani katika mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu ghasia na machafuko yaliyoungwa mkono na nchi ajinabi dhidi ya Iran.

Jana Alhamisi Naibu Mwaklishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa alisema kuwa ni fedheha kuona kuwa Washington imeugeuza Umoja wa Mataifa  “eneo la ukumbi wa michezo” kupitia madai yasiyo na msingi na hatua zake za kutumia vibaya maandamano ya amani nchini Iran.

Maandamano ya amani ya karibuni ya wananchi wa Iran yaligeuka na kuwa ghasia na machafuko kufuatia uingiliaji wa wazi wa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel. 

Mamluki wa nchi ajinabi na magaidi wenye silaha walivamia na kuharibu mali za umma, ikiwemo misikiti na miundombinu mbalimbali na kupelekea kuuliwa shahidi na kujeruhiwa raia na vikosi vya usalama. 

Kwa mujibu wa mamlaha husika za Iran, makumi ya raia na vikosi vya usalama wameuliwa shahidi katika ghasia za magaidi wenye silaha katika maeneo mbalimbali nchini. Idara za Intelijinsia za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimethibitisha kuwa mamluki hao walipatiwa msaada wa kijasusi, silaha, kiloijistiki na fedha na Washington na Shirika la Ujasusi la Israel (Mossad). 

Ujumbe wa Marekani ukiongozwa na Balozi Mike Waltz amedai kuwa machaguo yote yako mezani kwa jaili ya kushughulikai kile alichokiita ukandamizaji wa serikali.

Naye Naibu Mwaklishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameijibu Marekani na kuikosoa kwa kauli zake za upotoshaji na kinyume na uhakika wa mambo. Katika hotuba yake kwa mkutano wa dharura wa jana wa Baraza la Usalama, Naibu Mwakilishi huyo wa Iran UN ameikosoa vikali Marekani kwa uwongo na kupotosha kwa makusudi ili kuficha “kuhusika kwake moja kwa moja katika kuchochea ghasia nchini  ili Iran itumbukie katika hali ya mchafukoge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *