#HABARI: Jeshi la Polisi mkoani Mtwara, kwa kushirikiana na Askari wa Wanyamapori, limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili kwa tuhuma za kupatikana na nyara za Serikali, ikiwa ni pamoja na meno ya tembo.

Watuhumiwa hao ni Ignas Aron Mponza, Mwalimu wa Shule ya Msingi Namitende, na Diksoni Ado, mkulima, wote wakazi wa Kijiji cha Nang’umbu, Wilaya ya Ruangwa, Mkoa wa Lindi.

Taarifa ya Jeshi la Polisi kupitia kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Issa Suleiman, inaeleza kuwa watuhumiwa waliondoka Wilaya ya Ruangwa wakiwa na meno ya tembo kwa kutumia Pikipiki aina ya TVS isiyo na namba za usajili, wakielekea Wilaya ya Masasi kwa lengo la kuuza nyara hizo.

Watuhumiwa hao walikamatwa ndani ya nyumba ya kulala wageni, wakiwa wanamsubiri mteja waliokuwa wamekubaliana naye kufanya biashara hiyo haramu.

Jeshi la Polisi limesema uchunguzi unaendelea na watuhumiwa watafikishwa Mahakamani mara baada ya taratibu za kisheria kukamilika.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *