#HABARI: Watumishi wawili wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoani Njombe, Hadson Mwitagila (41) ambaye ni Mhasibu na Abdul Hussein (33) ambaye ni Msoma Mizani, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Njombe.

Washitakiwa hao wanakabiliwa na kosa la kushawishi na kupokea rushwa ya shilingi laki nne na elfu hamsini (450,000) kutoka kwa dereva wa gari la mizigo ili wamsaidie baada ya gari lake kubainika kuzidisha uzito wa mbolea katika mizani ya Makambako.

Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Saidi Ng’ande, ameiambia Mahakama kuwa watuhumiwa hao walinaswa Januari 23, 2026, kufuatia mtego uliowekwa na taasisi hiyo baada ya dereva wa gari lenye namba T.857 ECC kuombwa fedha hizo.

Kitendo hicho ni kinyume na sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa, na kimehusishwa na eneo la mizani ya Makambako iliyopo kando ya barabara kuu inayounganisha mikoa ya Dar es Salaam na Mbeya.

Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mheshimiwa Matrida Kayombo, ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 10, 2026, itakapotajwa tena kwa ajili ya hatua nyingine za kisheria.

Aidha, Mahakama imetoa masharti ya dhamana ya shilingi milioni tatu kwa kila mshitakiwa pamoja na wadhamini wawili; ambapo washtakiwa walionywa kuwa wakishindwa kutimiza masharti hayo wataendelea kubaki rumande mpaka tarehe ya kesi yao itakapotajwa tena.

Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *