#HABAI: Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) imeendesha zoezi la uhakiki wa uthamini wa mali kwa wananchi, walioguswa na Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Katumba–Lupaso yenye urefu wa kilomita 35.3, mkoani Mbeya.
Mradi huo ni sehemu ya tatu ya ujenzi wa Barabara ya Katumba–Mbambo–Tukuyu yenye jumla ya kilomita 79, unaotekelezwa na Serikali kupitia TANROADS kwa lengo la kuboresha miundombinu ya usafiri na kukuza uchumi wa wananchi wa eneo hilo.
Zoezi la uhakiki linafanyika ili kuthibitisha taarifa za uthamini kwa wananchi waliomo kwenye mpango wa fidia, kuhakikisha haki, uwazi na ushirikishwaji wa wananchi kabla ya kuendelea na utekelezaji wa mradi.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mthamini Mwandamizi kutoka TANROADS, FRV Anna Deo Urassa, amesema kuwa usanifu wa barabara katika baadhi ya maeneo umeingia kwenye ardhi za wananchi, hivyo kwa mujibu wa sheria wananchi hao wanastahili kulipwa fidia.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.