#HABARI: Mbunge wa Jimbo la Kivule lililopo Mkoani Dar es Salaam, Ojambi Massaburi, amesema Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi nzuri iliyoleta mageuzi makubwa nchini, ikiwemo kuvuna pesa nyingi kupitia gawio la Mashirika kwa Serikali na kuwekeza kwenye Mashirika yasiyo ya kiserikali.
Massaburi amesema hayo wakati akichangia mjadala unaohusu hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Bunge la 13.
“Kutokana na maarifa ya Mhe. Rais ilimpelekea kuvuna pesa nyingi za gawio la Serikali kutoka Bilioni 637 mpaka Trilioni 1.028 mwaka 2024/2025, tumeona Serikali imewekeza katika Mashirika yasiyo ya kiserikali tumepata ongezeko kutoka Bilioni 153 mwaka 2021 mpaka Bilioni 263 mwaka 2024/2025 ongezeko la 72%”
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania