#HABARI: Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limefanya ukaguzi wa kitaalamu katika maeneo ya Tabata na Kimara jijini Dar es Salaam, kufuatia malalamiko ya wateja mitandaoni kuhusu umeme kuisha haraka.

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, Bi. Irene Gowelle, aliongoza timu ya wataalamu, ambapo walibaini kuwa mita zote zilizokaguliwa ziko salama na zinafanya kazi kwa usahihi, kinyume na hofu iliyokuwa imetanda.

Matokeo ya ukaguzi huo yamebaini kuwa chanzo kikuu cha umeme kuisha haraka kwa wateja walalamikaji ni uchakavu wa mifumo ya nyaya (wiring) ndani ya nyumba zao. Katika kisa kimoja Tabata, iligundulika kuwa hitilafu ya wiring ilisababisha upotevu wa uniti mbili kila siku, hali iliyomgharimu mteja shilingi 30,000 za ziada kwa mwezi bila yeye kujua kuwa umeme ulikuwa unavuja.

Aidha, TANESCO imebaini kuwa matumizi holela ya nishati hiyo, ikiwemo kuwasha taa mchana na kutumia vifaa vya kizamani visivyo na ufanisi, huchangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa gharama.

Bi. Gowelle amewashauri wateja kufanya jaribio la kuzima vifaa vyote kwa saa nne ili kuona kama mita inaendelea kusoma, jambo litakalosaidia kubaini kama kuna uvujaji wa umeme kwenye mfumo wa wiring wa ndani.

Shirika limetoa wito kwa umma kuacha kusambaza taarifa zisizothibitishwa na badala yake wawasiliane na TANESCO moja kwa moja wanapohisi kuna changamoto. Lengo ni kuhakikisha wateja wanapata ufumbuzi wa kitaalamu na elimu ya matumizi fanisi ya nishati, jambo litakalosaidia kupunguza gharama zisizo za lazima na kuimarisha usalama wa mifumo ya umeme majumbani.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *