‎ #HABARI: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhe. Patrobas Katambi, amesema Tanzania imeendelea kuwa miongoni mwa nchi salama Barani Afrika, kutokana na uimara wa Jeshi la Polisi na ushirikiano wake na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.

‎Akizungumza jijini Dodoma katika ziara yake ya kwanza kutembelea Makao Makuu ya Jeshi la Polisi tangu alipoteuliwa kuongoza wizara hiyo, Waziri Katambi amesema hali ya usalama nchini ni thabiti na Serikali itaendelea kuimarisha mifumo ya ulinzi ili kulinda amani iliyopo.

‎Ameongeza kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa wa Jeshi la Polisi katika kulinda maisha ya watu na mali zao, pamoja na kuhakikisha sheria zinazingatiwa kwa haki.

‎Katika ziara hiyo, Waziri Katambi aliambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Ayoub Mohamed Mahmoud, na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara hiyo, Miriam Mmbaga.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *