
Jeshi la Nigeria limesema siku ya Jumapili nkuwa vikosi vyake vilimuua kamanda wa Boko Haram na wapiganaji wengine 10 wa kundi hilo la kigaidi wakati wa operesheni kaskazini mashariki mwa nchi.
Katika taarifa, jeshi linasema kuwa vikosi vyake ilifanya operesheni hiyo katika msitu wa Sambisa ulioko jimbo la Borno.
Kamanda huyo aliyeuawa ametajwa kuwa ni Abu Khalid, ambaye alikuwa wa pili kwenye uongozi wa Boko Haram msitu wa Sambisa. Alielezewa kuwa mtu muhimu ndani ya kundi hilo la kigaidi ambaye alikuwa na majukumu ya kuratibu operesheni na mipango msitu wa Sambisa.
Hakuna aliyesemekana kuuawa upande wa wanajeshi wa Nigeria, taarifa hiyo iliongeza, kuwa operesheni dhidi ya ugaidi zinaendelea katika maeneo ya misitu kote kaskazini mashariki.