
Amesema ushirikiano wa kuunda ajira nzuri nchini Ethiopia, utawazuwia raia kuondoka nchini humo huku ushirikiano wa sheria ukiwa muhimu ili kukabiliana na magenge ya wanaofanya biashara haramu ya usafirishaji wa binaadamu.
Amesema hatua hiyo pia itauharakisha mchakato wa kuwarejesha nyumbani wahamiaji haramu kutoka Ethiopia wasio na haki ya kuishi Uingereza.
Waziri huyo wa mambo ya nchi za nje wa Uingereza Yvette Cooper, amesema nchi yake pia inania ya kuimarisha biashara na nchi hiyo ya Pembe ya Afrika ili watu wake wapate maisha mazuri nyumbani kuliko kutumia njia hatari za kufika Ulaya.