Idadi ndogo tu ya watu wapatao 50 kutoka kila upande ndio watakaoruhusiwa kutumia kivuko hicho kila siku, huku majadiliano yakiendelea juu ya hatua za kiusalama na kiuendeshaji.

Israel imesema wapalestina 42,000 pekee waliokimbia Gaza wakati wa vita ndio wataruhusiwa kurejea Gaza kupitia kivuko hicho.

Lakini kwa mujibu wa wizara ya afya kwenye Ukanda huo, kiasi cha wagonjwa 20,000 wanangojea kuingia Misri kwa matibabu, huku 440 kati yao wakiwa na hali mbaya kabisa. Wagonjwa 4,000 wa saratani na watoto 4,500 wamo pia kwenye orodha ya dharura. Hata hivyo wapalestina wanatumai operesheni kupitia kivuka hicho itaendeshwa salama na kuridhia watu wengi zaidi kupita kama anavyosimulia mkaazi wa Gaza Jihad al-Arja.

“Tunatumaini mambo yatakwenda vizuri na kwamba kuingia na kutoka kwa watakaotumia kivuko hiki  kutakuwa rahisi, kwa sababu kuna idadi kubwa ya wagonjwa na wazee hapa ambao wanaoteseka kutokana na magonjwa walionayo na wanahitaji matibabu ya haraka na wanahitaji kusafiri kwenda Misri au nje ya nchi.”

Kufunguliwa kwa kivuko hicho muhimu kwa maisha ya Wapalestina kilichofungwa kwa zaidi ya mwaka sasa ni sehemu ya kile kiitwacho “mpango wa amani wa Rais Trump kwa Gaza”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *