KMC vs SIMBA: “Presha haiwezi kuondoka”
Kocha wa KMC, Mohamed Abdallah ‘Bares’ anasema kukosekana kwa matokeo mazuri kwenye mechi zao zilizopita katika NBC Premier League kunaifanya timu hiyo iwe na presha japo timu yao imekuwa ikiimarika siku hadi siku.

Kocha huyo anasema mchezo wa kesho wanauendea kwa lengo la kupunguza presha kwa mashabiki.

Kwa upande wake mchezaji Daruweshi Saliboko anasema kama kila mchezaji atafuata maelekezo kwa asilimia kadhaa, basi watafanya vema katika mchezo wa kesho.

Mechi itapigwa katika dimba la KMC Complex, saa 1:00 usiku LIVE #AzamSports1HD

(Imeandikwa na @allymufti_tz)

#NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdate #ImenogaZaidi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *