Wakala wa Vipimo (WMA) imewahimiza wananchi kote nchini kuwa na uelewa wa haki yao ya msingi ya kuhoji na kuthibitisha usahihi wa vipimo wanapofanya manunuzi dukani au katika eneo lolote linalotumia mizani na vipimo.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Wakala wa Vipimo (WMA) Bi. Veronica Simba wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoa elimu ya matumizi sahihi ya vipimo kwa wanafunzi wa Shule ya Mfano ya Dkt. Samia Dodoma Sekondari ambapo amesisitiza kuwa kila mwananchi ana wajibu na haki ya kuhakikisha anapata thamani halisi ya fedha yake.

Hapa Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Dodoma, Bw. Said Mussa, anaeeleza hatua kali za kisheria dhidi ya mtu au mfanyabiashara atakayebainika kutoa vipimo visivyo sahihi.

Kwa upande wao Wanafunzi pamoja na mwalimu kutoka Shule ya Mfano ya Dkt. Samia Dodoma Sekondari wanaeleza namna walivyoipokea elimu hiyo na jinsi itakavyowasaidia kutambua haki zao pindi wanapofanya manunuzi.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *