Jeshi la polisi mkoani Ruvuma linawashikilia watu watatu kwa kutuhuma za kumtapeli wakala wa fedha Paulo Dainet Akweso shilingi milioni 147 mkazi wa kata ya Bombambili Manispaa ya Songea baada ya kumlaghai kuwa wanataka kumpatia utajiri wa haraka hivyo awape kiasi cha fedha ili ziweze kufanyiwa dawa kwa lengo la kupata utajiri mkubwa .
Akitoa taarifa kwa umma kamanda wa Polisi mkoa kamishna msaidizi mwandazi Marco Chillya amesema tukio hilo limetokea februari 5,2026 majira ya sita mchana katika nyumba ya kulala wageni.
(Feed generated with FetchRSS)