Minong’ono ilimfuata nje ya mtandao na hata mtandaoni. Matusi na unyanyasaji vililipuka bila kudhibitiwa: maoni, dhihaka, watu kutumiana picha hizo. Hakuwahi kutoa ridhaa kwa lolote kati ya hayo. Hilo halikumzuia yeyote.

Ndani ya dakika chache, maelfu ya watu walikuwa wameona maudhui hayo. Na ndani ya saa chache, mamilioni. Ndoto mbaya ilikuwa ndiyo inaanza.

Siku zilipita kabla ya majukwaa ya mtandaoni kuchukua hatua. Kufikia wakati huo, picha zilikuwa tayari zimeonwa, kuhifadhiwa na kusambazwa tena.

 Alibaki akijiuliza: Nitamripoti nani? Je, kuna yeyote atakayeniamini? Je, waliofanya hivi watawajibishwa? Au lawama zitaangukia kwangu?

Huu ndio uhalisia kwa maelfu ya wanawake na wasichana kila siku. Picha zilizohaririwa na akili mnemba au AI, kwa lugha ya kiingereza, Deepfakes  zinaharibu maisha halisi, na haki bado haipatikani kwa manusura wengi.

Mwanamke anatumia smartphone yake, labda akishirikiana na maudhui ya mitandao ya kijamii, akikazia masuala ya unyanyasaji wa mtandao na unyanyasaji wa kina.

© Unsplash/Finn

Deepfakes ni picha, video, au sauti ambazo zimedhibitiwa au kuzalishwa kwa kutumia teknolojia za AI.

Je Deepfakes ni nini? (Iwe kwenye box)

Deepfakes ni picha, sauti au video zilizohaririwa kwa teknolojia ya akili mnemba (AI) ili kuonekana kana kwamba mtu amesema au amefanya jambo ambalo hakuwahi kulisema au kulifanya. Teknolojia hii si mpya. Hata hivyo, kutumika kwake kama silaha dhidi ya wanawake na wasichana ni jambo jipya zaidi, na linaongezeka kwa kasi kubwa.

Janga la kutowajibishwa: Mara chache sana watengenezaji wa maudhui haya kuwajibishwa

Licha ya madhara makubwa, mashtaka ni machache, majukwaa hushindwa kuchukua hatua, na manusura huumizwa tena pale wanapotafuta msaada. Kwa nini kuna pengo la uwajibikaji?

1. Sheria hazijaendani na teknolojia

Nchi nyingi hazina sheria za kushughulikia unyanyasaji mtandaoni, na chache zaidi zinatambua maudhui hayo dhalili yanayotengenezwa na AI. Sheria nyingi za picha za ngono zinazosambazwa kwa visasi kutoka kwa wapenzi bila ridhaa ya mwingine au “revenge porn” kwa lugha ya kiingereza ziliandikwa kabla ya teknoloji ya sasa, zikitoa mianya ya kisheria.

Baadhi ya maeneo kama Muungano  wa Ulaya na Marekani zimeanza kuchukua hatua, lakini bado ni nadra. Ukosefu wa ufafanuzi na msisitizo wa ridhaa huwapa wahalifu nafasi ya kukwepa adhabu.

2. Utekelezaji siku za awali

Hata pale sheria zilipo, utekelezaji ni dhaifu. Uchunguzi huhitaji utaalamu wa kidijitali, ushirikiano wa kimataifa na msaada wa majukwaa — rasilimali ambazo mara nyingi hazitoshi. Ushahidi hupotea haraka, wahalifu hujificha kwa majina bandia au mipaka ya nchi, na mifumo ya haki hushindwa kuendana na kasi ya teknolojia.

3. Manusura hunyamazishwa kabla ya kuripoti

Kuripoti kunawalazimu manusura kuonesha picha zao kwa mamlaka, kuhatarisha sifa zao na kukumbana na unyanyapaa au lawama. Wengi huchagua kunyamaza na kujilinda kwanza, jambo linalofanya wahalifu wasiwajibishwe.

Smartphone inayoonyesha ubongo wa digital kwenye skrini yake, iliyowekwa juu ya kompyuta ndogo, ikiwakilisha akili bandia na teknolojia ya kizazi kijacho.

© Unsplash/Aidin Geranrekab

Akili Mnemba sasa inabadilisha sekta ya simu ya rununu.

4. Majukwaa yanashindwa kuwasaidia manusura

Kampuni za teknolojia mara nyingi huchelewa kuondoa maudhui, huwa na taratibu zisizo wazi, na hutoa majibu ya kimashine. Mzigo wa kufuatilia na kuripoti kila nakala huachwa kwa manusura, huku maudhui yakiendelea kusambaa.

Kutafuta haki hutumbukiza manusura kwenye madhara zaidi

Manusura wanaoripoti hukumbana na maswali ya kuumiza na uchunguzi unaowalenga wao badala ya wahalifu. Madhara ya mtandaoni mara nyingi huenea hadi nje ya mtandao, yakihusisha vitisho na mashambulizi halisi.

Haki inahitaji nini

Manusura wanahitaji kuaminiwa, wahalifu wawajibishwe, na wapate msaada wa kisheria na kisaikolojia. Pia wanahitaji serikali na majukwaa kuchukua hatua za kuzuia unyanyasaji kabla haujatokea.

Hatua za haraka zinazohitajika

  • Sheria wazi zinazotambua maudhui haya dhalili yanayotumia teknolojia ya AI na kuzingatia ridhaa.
  • Mifumo imara ya haki yenye rasilimali na ushirikiano wa kimataifa.
  • Uwajibikaji wa majukwaa kwa kuondoa maudhui haraka na kushirikiana na mamlaka.
  • Msaada wa kweli kwa manusura, ikiwemo msaada wa kisheria bila gharama.
  • Elimu ya kidijitali na ridhaa ili kuzuia unyanyasaji mapema.

Unyanyasaji kupitia maudhui haya dhalili yanayotengenezwa na akili mnemba ni sehemu ya wimbi kubwa la ukatili wa kidijitali dhidi ya wanawake na wasichana.

UN Women inasema vitendo hivi vinaongezeka, vina sura ya kijinsia, na mifumo ya ulinzi inashindwa. Hali hii lazima ibadilike na ibadilike sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *