
Nchini Afrika Kusini, uzinduzi wa kampeni ya mtandaoni inayotaka Patrice Motsepe, bilionea na rais wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), aweze kuchaguliwa mwaka wa 2027 kama mkuu wa ANC unasababisha msukosuko ndani ya chama tawala.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu mjini Johannesburg, Claire Bargelès
Nchini Afrika Kusini, uchaguzi mkuu ujao bado uko mbali, umepangwa kufanyika mwaka wa 2029. Lakini wakati huo huo, vyama vinateua watu wapya kushinikilia nafasi za viongozi wao. Chama cha African National Congress (ANC), chama kilicho madarakani tangu mwisho wa ubaguzi wa rangi, kinatarajiwa kufanya uchaguzi wa ndani mwaka wa 2027 ili kumchagua mrithi wa Cyril Ramaphosa, mkuu wa sasa wa nchi, ambaye anafikia mwisho wa mihula yake miwili. Na kampeni ya mtandaoni inayozua gumzo imeanza, ikilenga kutangaza uwezekano wa kugombea kwa Patrice Motsepe, 64, Mwebyekitiwa sasa wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), ingawa bilionea huyo hadi sasa amesisitiza kuwa hana nia yakuwania kwenye nafasi hiyo.
Haijulikani haswa ni nani anayeongoza kampeni hii, inayoitwa “PM27.” Kifupi hiki kinatumia herufi za kwanza si za Makamu wa Rais wa Afrika Kusini Paul Mashatile, mrithi mtarajiwa wa Cyril Ramaphosa, bali zile za Patrice Motsepe, kwa kutarajia uchaguzi wa ndani wa ANC uliopangwa kufanyika mwaka ujao.
Tovuti imezinduliwa ili kukusanya mafanikio ya gwiji huyu wa madini, ambaye ni shemeji kwa uhusiano wa kindoa na kiongozi wa sasa wa Afrika Kusini. Kulingana na wapiga debe wake, mmwenyekiti wa mpira wa miguu Afrika ndiye “kiongozi anayeaminika zaidi, anayeunganisha, na mwenye maono ya kuongoza ANC.” Mpango huu umeibua maswali, na Patrice Motsepe, ambaye ni msiri sana kila wakati, bado hajaujibu.
“Wasiwasi mkubwa” kwa ANC
Kinyume chake, chama husika cha siasa kimelazimika kuzungumza: katika taarifa, msemaji wa ANC alishiriki “wasiwasi mkubwa” wa cama cha African National Congress kuhusu hatua hii na akabainisha kwamba kampeni za mapema zimepigwa marufuku na kamati ya ndani. Kulingana naye, makundi yote lazima yahamasishwe kujiandaa kwa uchaguzi wa ndani, ambao utafanyika ndani ya mwaka mmoja.
Ndani ya chama cha Democratic, chama cha pili kisiasa kwa ukubwa nchini, wanasema suala la uongozi wa chama pia linaibuliwa, huku kiongozi anayeondoka madarakani, John Steenhuisen, akijiondoa. Meya wa Cape Town, Geordin Hill-Lewis, tayari ametangaza kugombea kwake uchaguzi wa ndani mwezi Aprili.