Umoja wa Mataifa umeonya kuwa huenda kipindi cha El Nino kikarejea tena baadae mwaka huu, wakati huu majira ya baridi ya La Nina yakitoweka.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa shirika la umoja wa mataifa la hali ya hewa, kupungua kwa majira ya La Nina kunatarajiwa kusababisha mvua kubwa za El Nino kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Shirika hilo linasema, katika kipindi cha Aprili hadi Juni, kuna uwezekano wa hali ya wastani kuongezeka hadi asilimia 70, ambapo pia kati ya mwezi Mei hadi Julai kuna uwezekano wa hali hii ya wastani kushuka hadi asilimia 60 huku kuwepo kwa El nino kukiongezeka hadi asilimia 40.

Mkurugenzi wa shirika hilo, Celeste Saulo, amesema wataalamu wake wanaendelea kufuatilia hali hiyo ili kusaidia kutoa maelekezo muafaka, ambapo ameongeza kuwa El Nino yam waka 2023 na 2024, ilikuwa miongoni hali tano mbaya zaidi za kimazingira na ilichangia ongezeko la joto mwaka 2024.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *