Israel imetangazaleo  Jumatano, Machi 4, kwamba imezindua “wimbi kubwa” la mashambulizi mapya dhidi ya Iran, huku vita vya Mashariki ya Kati vikiingia siku yake ya tano. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Iran inaendelea kulipiza kisasi kwa kurusha makombora dhidi ya Israel na katika nchi za Ghuba. Athari inayoongezeka ya mzozo wa kikanda inasababisha bei ya mafuta kupanda na kutisha masoko, haswa barani Asia, ambapo soko la hisa la Seoul lilisitiishwa baada ya kushuka kwa kasi.

Kwa upande mwingine Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliionya Israel siku ya Jumanne dhidi ya operesheni ya ardhini nchini Lebanon, ambayo aliiita “kuongezeka kwa hatari na kosa la kimkakati,” huku pia akisema kwamba Hezbollah ilifanya “kosa kubwa” kwa kuwa wa kwanza kuishambulia Israel. 

Wakati huo huo, alitangaza uimarishaji wa kijeshi kwa Mashariki ya Kati inayokumbwa na vita, ikiwa ni pamoja na meli kubwa ya kubeba ndege Charles de Gaulle na kikosi chake cha meli za kivita, ambazo “zitasafiri” kuelekea Mediterania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *