
Israeli imezindua mashambulizi mapya dhidi ya Lebanon siku ya Alhamisi, Machi 5, ikifanya mashambulizi ya anga katika miji kadhaa ya mpakani kusini mwa nchi. Wakati huo huo, Iran imezindua mashambulizi mengine ya makombora dhidi ya Israel, kulingana na jeshi la Israel na vyombo vya habari vya serikali ya Iran.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Baada ya utulivu wa zaidi ya saa saba, jeshi la Israel limetangaza asubuhi kwamba liimeawasha ulinzi wake wa anga na kuanzisha mashambulizi mapya dhidi ya mji wa Tehran na viunga vyake. Washington na Israel zinaunganisha nguvu zao pamoja dhidi ya Iran ambayo wanaiona kuwa imedhoofika sana.
Manowari ya Marekani ilizamisha meli ya Iran karibu na pwani ya Sri Lanka katika Bahari ya Hindi siku ya Jumatano, na kuwaua angalau mabaharia 87 na kusababisha kadhaa kutojulikani walipo. Meli ya Iran ni ya kwanza kuzamishwa na manowari ya Marekani tangu Vita vya Pili vya Dunia. Mamlaka ya Sri Lanka ilishuhudia kuwasili kwa meli ya pili ya kivita ya Iran karibu na maji yake siku ya Alhamisi asubuhi.
Meli ya mafuta ya Marekani “ilipigwa na kombora kaskazini mwa Ghuba ya Uajemi,” Walinzi wa Mapinduzi wamesema katika taarifa iliyosomwa kwenye televisheni ya serikali, bila kutoa maelezo zaidi.
Wakati huo huo Baraza la Seneti la Marekani siku ya Jumatano lilikataa kupunguza mamlaka ya Donald Trump katika vita dhidi ya Iran, azimio la matokeo hayo likishindwa kutokana na uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa walio wengi wa Republican.
Kulingana na shirika rasmi la habari la Iran, kampeni za mabomu zinazofanywa na Marekani na Israel zimewaua watu 1,045 tangu Jumamosi, Februari 28. Siku iliyotangulia, Shirika la Hilali Nyekundu liliripoti idadi ya vifo 787. Kulingana na jeshi la Marekani, karibu malengo 2,000 yalipigwa katika siku nne za kwanza za mzozo. Nchini Lebanon, mashambulizi ya anga ya Israel yamewaua watu 72 tangu siku ya Jumatatu.