Takriban watu 700,000 wakimbia makazi yao Lebanon huku mgogoro Mashariki ya Kati ukizidiTakriban watu 700,000 wakimbia makazi yao Lebanon huku mgogoro Mashariki ya Kati ukizidi

Israel – Mamlaka za afya zimeripoti kuwa watu karibu 2,000 wamejeruhiwa tangu mapigano yaanze, huku mtu mmoja akiuawa baada ya kombora kuanguka katikati mwa nchi hiyo hii leo. 

Iran – Yenyewe imesema zaidi ya raia 1,330 wameuawa kutokana na mashambulizi ya Israel na Marekani.

Sehemu katika Beirut, Lebanon inayoonyesha familia za wakimbizi wanaoishi mitaani. Mbele, mwanamume analala kwenye benchi, wakati mwanamke aliyevaa suti ya kijani na hijab ameketi karibu na mtoto katika gari. Vitu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na hookah, vimetapakaa karibu nao. Watu wengine wanaonekana nyuma kwenye barabara ya jiji.

© UNICEF/Dar al-Mussawir

Wanafamilia wanapumzika barabarani mjini Beirut, Lebanon, baada ya kutoroka nyumba yao kutokana na amri ya kuhamishwa.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yazungumza

WFP – Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani imeonya kuwa vita hivyo vinaweza kuongeza uhaba wa chakula. Mashambulizi dhidi ya usafiri wa majini katika Mlango wa Hormuz yameathiri biashara ya kimataifa ya mafuta na mbolea, hali inayoweza kuongeza bei ya chakula duniani.

Shirika hilo linasema Lebanon na Iran tayari zilikuwa na viwango vya juu vya ukosefu wa chakula kabla ya vita, na mgogoro huu unaweza kuongeza mateso kwa mamilioni ya watu.

UNICEF Shirika la Umoja wa Mataifa linalihusika na masuala ya watoyo  katika taarifa yao wameeleza kuwa, kati ya waliokimbia makazi yao nchini Lebanon takriban watoto 200,000 wameathirika. Idadi hiyo inaongezeka juu ya maelfu ya watu waliokuwa tayari wamehamishwa makazi kutokana na misukosuko iliyotokea siku za nyuma.

Mapigano hayo yameongezeka kufuatia mashambulizi ya Israel na Marekani dhidi ya Iran mwishoni mwa wiki, mashambulizi ya kulipiza kisasi kutoka Iran dhidi ya Israel, pamoja na mashambulizi ya Israel dhidi ya kundi la Hezbollah nchini Lebanon.

OCHAShirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada ya kibinadamu limeeleza kuwa, watu 294 wameuawa na zaidi ya 1,000 kujeruhiwa nchini Lebanon katika siku nane za mwanzo za vita. Mnamo Machi 7,2026 watu 41 waliuawa katika operesheni moja ya jeshi la Israel katika mji wa Nabi Sheet mashariki mwa Lebanon.

Mashambulizi ya anga pia yameongezeka katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo, huku Israel ikitoa tena amri ya watu kuhama maeneo ya kusini mwa Mto Litani pamoja na vitongoji vya kusini mwa mji mkuu wa Beirut.

Mratibu wa misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa, Tom Fletcher, ameonya kuwa vita hivyo vinaweza kuwa na athari kubwa zaidi kwa nchi nyingine ambazo tayari zinakabiliwa na changamoto kubwa za kibinadamu, ikiwemo Afghanistan na Pakistan. Ameeleza pia kuwa migogoro mingine kama ile ya Sudan, Sudan Kusini na Ukraine inaweza kupoteza uangalizi wa kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *