
Russell alisema mawazo yake yako pamoja na familia, wapendwa na wafanyakazi wenzake wa UNICEF wanaoomboleza kifo cha mwenzake huyo. Alisisitiza kuwa raia, wakiwemo wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu wanaofanya kazi ya kusaidia jamii zilizo katika hatari, hawapaswi kamwe kulengwa katika mashambulizi.
Mashariki mwa DRC, hususan katika eneo la Goma, imeendelea kushuhudia mapigano kati ya makundi yenye silaha na majeshi ya serikali, hali inayowaweka raia na wahudumu wa misaada katika hatari kubwa.
Kwa mujibu wa duru za habari kutoka Goma DRc mfanyakazi huyo ameuawa asubui ya leo machi 11,2026 mjini Goma katika shambulizi la ndege isiyo na rubani au droni mashariki mwa jamuhuri yakidemocrasia ya kongo.
Droni hiyo ilikuangusha bomu kwenye nyumba mfanya biashara wa kampuni ya TOYOTA.
Hadi sasa hakuna yeyote aliyedai kuhusika na shambulizi hilo na taarifa zaidi kuhusu mauaji hayo zinatarajiwa.