
DAR ES SALAAM: SHEREHE za Sikukuu ya Eid el-Fitri zinatarajiwa kuwa Machi 20 au 21. 2026 kutegemea mwandamo wa mwezi.
Taarifa iliyotolewa leo Machi 12, 2026 na Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Alhaji Nuhu Mruma imesema swala ya Idd kitaifa itaswaliwa Msikiti wa Mfalme Mohamed VI, Kinondoni, Dar es Salaam.
“Swala ya Eid itaswaliwa Msikiti wa Mfalme Mohamed VI uliopo Makao Makuu ya BAKWATA Kinondoni kuanzia saa 1:30 asubuhi, huku Baraza la Eid likifanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) kuanzia saa 9:00 mchana,” imefafanua taarifa hiyo na kuongeza kuwa mgeni rasmi katika Baraza la Idd anatarajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan.