Dar es Salaam. Benki ya CRDB imezindua kampeni ijulikanayo kwa jina la “Fainali Ndo Mpango na TemboCard Visa” ambapo jumla ya washindi 10 watashinda tiketi ya kushuhudia mechi za fainali ya Kombe la dunia nchini  Marekani na Canada.

Mbali ya Marekani na Canada, michuano ya Kombe la dunia ambayo imepangwa kuanza Juni 11 mpaka Julai 19, pia yanafanyika nchini Mexico.

Akizungumza wakati wa uizinduzi jana, Mkurugenzi wa Wadogo na wa Kati wa benki ya CRDB Bonaventura Paul alisema kuwa kinachotakiwa kufanywa na wateja wa CRDB ni kufanya  miamala angalau kuanzia 30 kwa kutumia Tembo CardVISA.

Alisema pia wateja wao wanaweza kutumia TemboCard Visa Debit, Prepaid Card au Credit Card kufanya malipo ya huduma au bidhaa wanazonunua wataingia moja kwa moja kwenye droo ya ushindi.

Bonaventura alisema kuwa kati ya washindi hao 10, wanne watapata fursa ya kuona mechi ya fainali nchini Marekani ambapo washindi sita watapata fursa ya kuona mechi za hatua ya makundi nchini Canada.

Alisema kuwa Benki ya CRDB itagharimia gharama zote ikiwa pamoja na taratibu za safari. Alisema kuwa mbali ya washindi hao 10, pia kutakiwa na washindi wengine 10 ambao watazawadiwa televisheni kubwa ya kisasa ya inchi 85 na king’amuzi.

Alisema kuwa kutakiwa na jumla ya droo tatu ambapo droo ya kwanza itafanyika Aprili 4 ambayo washidni wanne wa mechi ya fainali watapatikana na pia washindi watatu wa televisheni na king’amuzi. Droo ya pili itafanyika Mei 12 ambapo washindi wa tatu wa kwenda Canada kuona mechi za hatua ya makundi watapatikana na washindi watatu wa televisheni na king’amuzi watapatikana.

Droo ya mwisho itafanyika Juni 11 ambayo itatoa washindi watatu wa mechi za hatua ya makundi nchini Canada na washindi wanne wa televisheni watapatikana.

“Lengo kubwa ni kuhamasosha matumizi ya Tembo card visa katika kufanya malipo au manunuzi mbalimbali ya kidigitali.

Mpira wa miguu ni mchezo unaowaunganisha watu duniani kote bila kujali taifa, lugha au utamaduni wao. Kwa kulitambua hilo, sisi Benki ya CRDB tumeona ni muhimu kuwapa wateja wetu nafasi ya kuwa sehemu ya msisimko huo wa kimataifa kupitia mchezo huu pendwa duniani,” alisema Bonaventura

Kwa mujibu wa Bonaventura kwa sasa dunia inahamia kwenye mfumo wa malipo ya kidijitali hivyo Watanzania nao ni lazima waingie huko ili kuzitumia fursa zilizopo katika kununua au kuuza huduma na bidhaa kwani dunia imeshakuwa kama kijiji kwa watu kutoka popote duniani kununua huduma au bidhaa waitakayo bila kulazimika kuonana na muuzaji.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Visa Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda, Victor Makere amesema wanashirikiana na Benki ya CRDB kuwajumuisha Watanzania kwenye huduma za kidijitali za malipo kila wanapotaka kununua au kuuza huduma na bidhaa zao mtandaoni kama inavyofanywa katika mataifa mengine ulimwenguni.

“ Kwa sasa, duniani inapunguza utegemezi wa matumizi ya fedha taslimu hivyo Visa kwa kushirikiana na Benki ya CRDB  tunawapa wateja wetu njia salama, rahisi na yenye manufaa zaidi ya kufanya malipo pindi wanapofikiria kufanya malipo iwe ana kwa ana au wanaponunua bidhaa au huduma mtandaoni,” alisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *