Chanzo cha picha, Reuters
Effie Defrin, msemaji wa jeshi la Israel, ametoa taarifa kwa njia ya televisheni. Anasema jeshi la Israel bado lina “maelfu” ya shabaha za kushambulia Iran.
Defrin’s alinukuliwa na shirika la habari la Reuters akisema: “Tunatambua shabaha mpya kila siku.”
Wakati huohuo Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer na Rais wa Marekani Donald Trump wamejadili “hali inayoendelea katika Mashariki ya Kati na umuhimu wa kufungua tena Mlango-Bahari wa Hormuz ili kumaliza usumbufu wa usafirishaji wa mafuta duniani”.
Simu hiyo na Trump ilidumu kwa dakika 15, kulingana msemaji wa Downing Street.
Zaidi ya kujadili Mlango-Bahari wa Hormuz na rais wa Marekani, Starmer “pia alitoa rambirambi zake kwa wanajeshi wa Marekani ambao walipoteza maisha wakati wa vita”.