Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia Mwenyekiti wa Kijiji cha Mlangoni, Wilaya ya Siha, Ezekiel Mloli kwa tuhuma za kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha nne katika moja ya shule za sekondari wilayani humo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa na kueleza kuwa kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Amesema baada ya taarifa za tukio hilo kufikishwa kwa uongozi wa shule, mwanafunzi huyo alipelekwa katika Hospitali ya Wilaya kwa ajili ya uchunguzi wa kitabibu, ambapo ilibainika kuwa alikuwa na ujauzito wa wiki 17 na siku moja.
Kamanda Maigwa ameongeza kuwa mwanafunzi huyo alipofanyiwa mahojiano alimtaja Mwenyekiti wa Kijiji cha Mlangoni kuwa ndiye anayehusika na ujauzito huo.
Amesema taratibu za kisheria zitakapokamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
Jeshi la Polisi limetoa wito kwa jamii kuendelea kushirikiana na vyombo vya dola katika kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia na kulinda haki za watoto.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania