Rais wa Marekani, Donald Trump, amezihimiza nchi kama China na Japan kushiriki katika kulinda usalama wa Strait of Hormuz, akieleza kuwa Marekani inanufaika kwa kiwango kidogo sana na mafuta yanayopita katika njia hiyo.

Trump amesema kuwa Marekani hupata chini ya asilimia moja ya mafuta kupitia mlango huo wa bahari, huku mataifa kama China na Japan yakitegemea kwa kiwango kikubwa zaidi, hali inayofanya kuwajibika zaidi katika kuhakikisha usalama wake.

“Marekani tunapata mafuta kidogo sana kupitia Mlango Bahari wa Homuz, ni chini ya asilimia moja. Ila yapo mataifa kama Japan yanapata 95%, China 90% na South Korea 35%. Ndio maana nawaomba waje watusaidie kutatua suala la mlango ule wa bahari.”

Kauli hiyo imekuja wakati mvutano wa kiusalama ukiendelea katika eneo la Mashariki ya Kati, huku njia hiyo muhimu ya usafirishaji wa mafuta duniani ikiendelea kuwa kitovu cha taharuki ya Kimataifa.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *