#HABARI: Jeshi la Polisi mkoani Iringa limeyakamata na kuyashikilia mabasi mawili ya abiria yaliyokuwa yakisafirisha vifaranga vya kuku elfu 36 kutoka nchi jirani ya Malawi kinyume na taratibu.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, SACP Allan Bukumbi, amebainisha kuwa mabasi hayo yanayofanya safari kati ya Njombe, Mbeya na Dar es Salaam yamekiuka sheria za usafirishaji na kuhatarisha afya pamoja na usalama wa abiria waliokuwemo ndani ya magari hayo.
Aidha, Kamanda Bukumbi ameeleza kuwa kulikuwa na udanganyifu mkubwa wa takwimu kwani kibali cha ubebaji kilionyesha vifaranga elfu 16 pekee, wakati idadi halisi iliyokamatwa ni elfu 36.
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) mkoani Iringa imelaani kitendo hicho cha kugeuza mabasi ya abiria kuwa magari ya mizigo ya viumbe hai, ikisisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wamiliki na madereva waliohusika na ukiukwaji huo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.