#HABARI: Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga, amewataka watumishi wa Wizara ya Nishati kuongeza juhudi katika kukuza matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kuunga mkono ajenda ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi jijini Dodoma, Mhandisi Luoga amebainisha kuwa mafanikio ya Tanzania katika eneo hili yameanza kutambulika Kimataifa, ikiwemo kupongezwa na Rais wa Zimbabwe, Mhe. Emmerson Mnangagwa, katika mkutano wa hivi karibuni wa SADC.
Mkutano huo wa Baraza la Wafanyakazi umelenga kujadili na kupitisha mapendekezo ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2026/2027, ambapo Kamishna Luoga amewasisitiza wajumbe kuhakikisha vipaumbele muhimu vinatengewa fedha za kutosha.
Amesema kuwa sekretarieti ya SADC imezitaka nchi wanachama kuunga mkono mfano wa Tanzania, hatua inayothibitisha kuwa nchi imepiga hatua kubwa katika kuimarisha afya za wananchi na kupunguza uharibifu wa mazingira kupitia nishati mbadala.
Vilevile, Mhandisi Luoga amewakumbusha watumishi kuzingatia maadili ya utumishi wa umma kwa kufanya kazi kwa uzalendo, uadilifu, na kujiepusha na vitendo vya rushwa au utoro.
Amehitimisha kwa kuwapongeza watumishi hao kwa mchango wao uliowezesha Tanzania kuwa kinara wa nishati safi kusini mwa Afrika, huku akiwataka kuendelea kutoa huduma bora na za ufanisi kwa Watanzania ili kufikia malengo ya kitaifa yaliyowekwa.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.