#HABARI: Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, amesisitiza kuwa matumizi ya teknolojia ya kidijitali katika mfumo wa Mahakama ni nyenzo muhimu ya kuimarisha upatikanaji wa haki kwa wanawake na wasichana.
Akifungua mkutano wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) jijini New York, Dkt. Gwajima alibainisha kuwa usawa mbele ya sheria unahitaji mifumo ya haki inayofanya kazi kwa vitendo na inayofikiwa kwa urahisi na wananchi wote.
Dkt. Gwajima amekipongeza chama cha TAWJA kwa kuonyesha uzoefu wa Tanzania katika kuondoa vikwazo vya kisheria kupitia mifumo ya kidijitali, hatua inayosaidia kupunguza ucheleweshaji wa mashauri na gharama za kusafiri umbali mrefu kufuata huduma.
Alifafanua kuwa teknolojia hiyo inaimarisha usiri wa taarifa za waathirika wa ukatili wa kijinsia, jambo linalopunguza athari za kisaikolojia kwa manusura kwani hawalazimiki kujieleza mara kwa mara kutokana na kumbukumbu kutunzwa vizuri kielektroniki.
Aidha, Waziri ameeleza kuwa mifumo hiyo imesaidia ukusanyaji wa takwimu sahihi zinazozingatia jinsia, hali inayowezesha serikali kupanga sera na mikakati bora ya kisheria.
Ameshukuru mchango wa majaji wanawake nchini kwa uongozi wao uliotukuka ambao umeleta mageuzi makubwa yanayozingatia utu na uwajibikaji, huku akisisitiza kuwa mabadiliko hayo ni msingi imara wa kuhakikisha haki inatendeka kwa usawa na haraka kwa jamii nzima.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.