Katika taarifa iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi, Türk ameeleza kushtushwa na matukio yaliyoripotiwa nchini Ubelgiji, Uholanzi, Canada na Marekani .

“Nimeshtushwa na mashambulizi ya hivi karibuni ya chuki dhidi ya wayahudi yaliyolenga masinagogi na taasisi za Kiyahudi,” amesema.

Wito wa uchunguzi wa haraka na uwajibikaji

Türk amesisitiza umuhimu wa kuwawajibisha wahusika, akitoa wito kwa mamlaka za kitaifa kuchukua hatua za haraka na madhubuti.

Amesema “Ni muhimu sana mamlaka zichukue hatua za maana kuchunguza kwa haraka na kikamilifu mashambulizi haya ya kutisha na kuwafikisha wahusika mbele ya sheria”.

Ameonya kuwa kushindwa kuchukua hatua kunaweza kuchochea vitendo zaidi vya chuki na vurugu.

Uhuru wa kuabudu lazima ulindwe

Akisisitiza haki za msingi za binadamu, Türk amesema watu wote wanapaswa kuwa huru kuabudu bila hofu au vitisho vya aina yoyote.

“Kila mtu lazima aweze kuabudu imani yake bila hofu au vitisho vya aina yoyote”.

Taarifa hiyo inakuja wakati kuna hofu inaoongezeka duniani kuhusu kuongezeka kwa uhalifu wa chuki, huku Umoja wa Mataifa ukizitaka serikali kuimarisha ulinzi kwa makundi yaliyo hatarini na kulinda uhuru wa dini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *