#HABARI: Jeshi la Polisi leo Machi 19, 2026 limetoa tamko kuelekea sikukuu ya Eid El Fitri ambapo Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime ametoa tamko hilo kupitia ukurasa wao rasmi wa mtandao wa kijamii wa Instagram.
Tamko hilo linasema hivi; Karibuni tutaingia kipindi ambacho waumini wa dini ya Kiislamu watahitimisha Mfungo Mtukufu wa mwezi wa Ramadhani ambapo wataungana na Waislamu wenzao duniani kusherehekea Sikukuu ya Eid El Fitri.
Jeshi la Polisi linapenda kueleza kuwa, hali ya usalama ni shwari na limejipanga vizuri na litaendelea kushirikiana na viongozi katika ngazi ya Taifa, Mikoa Wilaya na Kata ili maeneo watakayopanga kufanyia swala ya Eid ikiwepo misikiti iendelee kuwa na amani, utulivu na usalama wakati wakimwomba na kumshukuru Mwenyezi Mungu.
Aidha, hali ya usalama itaendelea kuimarishwa katika maeneo ambayo familia, ndugu na marafiki wataona ni sahihi kwao kwenda kusherehekea Sikukuu ya Eid El Fitri.
Tahadhari inatolewa kwa wazazi na walezi wakati wanasherehekea sikukuu ya Eid kuwalinda watoto na kuhakikisha wanakuwa salama wakati wote kama sheria inavyoelekeza. Waepuke kuwaruhusu kwenda kutembea peke yao bila kuwa na uangalizi wa mtu mzima na mwenye akili timamu.
Kwa kufanya hivyo kutawaepusha watoto na madhara kama kufanyiwa vitendo vya kikatili, ajali za barabarani, hatari za kwenye fukwe na kupotea.
Aidha, tusisahau kuhakikisha tunaacha ulinzi mzuri kwenye makazi yetu kama itatulazimu kutoka ili kuepuka wizi au madhara mengine.”
INSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.