#HABARI: Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini mkoani Mtwara umetoa zawadi za vyakula kwa wafanyakazi wake 245 kama sehemu ya kusherehekea sikukuu ya Eid el-Fitr na kutambua mchango wao katika utoaji wa huduma za afya.

Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Dkt. Herbert Masigati, amesema hatua hiyo ni “mkono wa Iddi” wenye lengo la kuwatia moyo watumishi hao waendelee kufanya kazi kwa bidii na weledi wakati wote wa kuwahudumia wananchi wa kanda hiyo.

Kwa upande wao, baadhi ya wafanyakazi akiwemo Afisa Muuguzi, Perpetua Nandonde na Shafii Milela, wameushukuru uongozi kwa zawadi hizo wakisema ni kielelezo cha thamani wanayopewa kama watumishi.

Wamebainisha kuwa kitendo hicho kinajenga mshikamano na ari ya kufanya kazi ndani ya hospitali, huku wakiahidi kuendelea kutoa huduma bora za matibabu kwa jamii inayotegemea hospitali hiyo ya rufaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *