#HABARI: Wenyeviti wa serikali za vijiji vya Nambawala ‘A’ na ‘B’ wilayani Masasi, Emmanuel Swedi na Johnson Gideon, wameonya kuwa hawatasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wananchi wanaofanya shughuli za kilimo kando ya vyanzo vya maji.

Viongozi hao wametoa kauli hiyo wakati wa zoezi la upandaji miti katika chanzo cha maji cha Nambawala, wakisisitiza kuwa uharibifu huo unahatarisha upatikanaji wa maji kwa maelfu ya wakazi wa maeneo hayo na ni lazima udhibitiwe ili kunusuru rasilimali hiyo muhimu.

Katika kuelekea kilele cha Wiki ya Maji, Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka RUWASA Wilaya ya Masasi, Peter Mushi, amebainisha kuwa jumla ya miti 250 imepandwa kandokando ya chanzo hicho kama sehemu ya mkakati wa kuhifadhi mazingira.

Wakati baadhi ya wakulima wakikiri kuwepo kwa changamoto hiyo, RUWASA imetoa wito kwa jamii kuitunza miti hiyo na kuacha kabisa shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji ili kuhakikisha huduma hiyo inakuwa endelevu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *