#HABARI: Wanachama wa kikundi cha “Asante Mbeya” wamezua gumzo jijini Mbeya baada ya kupita mitaani na gari la matangazo wakishangilia kufanikiwa kurejesha mali zao, ikiwemo magari matatu, zilizokuwa zimechukuliwa isivyo halali na muasisi wao, Daniel Mwanakatwe (Danny FM).
Hatua hiyo imekuja baada ya wanachama hao kubaini udanganyifu na ubadhirifu wa fedha na rasilimali walizokuwa wakichangishwa na kiongozi huyo kwa ajili ya maendeleo ya kikundi.
Baada ya kugundua mchezo huo, wanachama walichukua hatua ya kufungua malalamiko katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ambapo uchunguzi ulisaidia kurejesha mali hizo mikononi mwao.
Tukio hilo limekuwa fundisho kwa vikundi vingine vya kijamii mkoani humo, huku viongozi wa kikundi wakisisitiza umuhimu wa uwazi na uadilifu katika kusimamia mali za wanachama ili kuepuka migogoro na hatua za kisheria.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.