#HABARI: Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, ameiambia jumuiya ya Kimataifa nchini India kuwa Tanzania inachukua hatua za kimkakati kuimarisha uzalishaji na usambazaji wa umeme ili kukidhi mahitaji ya uchumi unaokua.
Akizungumza katika mkutano wa Bharat Electricity Summit 2026, Mhandisi Mramba alitaja mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) wenye megawati 2,115 na mradi wa umeme jua wa Kishapu kuwa ni vigezo muhimu vya safari ya nchi kuelekea utoshelevu wa nishati.
Aidha, Mramba amesisitiza umuhimu wa maboresho ya gridi ya taifa kwa kutumia teknolojia za kisasa (smart grid) na kuunganisha mifumo ya umeme na nchi jirani ili kukuza biashara ya nishati kikanda.
Amesema hatua hizo zinalenga kuongeza ufanisi, uthabiti, na usalama wa nishati, huku serikali ikiendelea kufungua milango kwa sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika kuharakisha maendeleo ya sekta hiyo nchini.
Mwishoni, amebainisha kuwa nishati jadidifu inazidi kuwa sehemu muhimu ya mfumo wa umeme wa kisasa, hivyo kuna haja kwa taasisi za mipango na mashirika ya umeme kuimarisha uwezo wao wa kiufundi.
Mkutano huo umekuwa jukwaa muhimu kwa Tanzania kuelezea dira yake ya nishati, ikilenga kutumia teknolojia za kisasa na ushirikiano wa kimataifa ili kuhakikisha huduma ya umeme inakuwa chachu ya mageuzi makubwa ya kijamii na kiuchumi.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.