Vita vya Mashariki ya Kati vimeendelea, huku Iran ikirusha makombora kulenga vituo vya nishati ya gesi nchini Qatar na Saudi Arabia, baada ya Israeli kushambulia kituo kikubwa cha gesi nchini Iran cha Pars.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya nishati nchini Qatar, imesema kituo chake cha gesi kilichopo Ras Laffan kimeharibiwa vibaya, kufuatia shambulizi la makombora kutoka Iran.

Kufuatia kitendo hicho cha Tehran, Qatar imewafukuza wawakilishi wa jeshi la Iran nchini mwake.

Nchi ya Falme za Kiarabu nayo imeagiza kufungwa kwa kituo chake cha gesi cha Habshan jijini Abu Dhabi, huku Saudi Arabia ikisema  vituo vyake viwili vya kusafisha mafuta vimeshambuliwa na Iran.

Naye, rais Donald Trump amesema Marekani haikufahamu kuwa Israel ilishambulia kituo cha gesi nchini Iran, na kutishia  mashambulio makubwa yatafanyika katika kituo cha gesi Kusini mwa Pars, iwapo Tehran itashambulia tena kituo cha gesi nchini Qatar.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, kiongozi huyo wa Marekani ameongeza kuwa Israeli haitashambulia tena kituo cha gesi nchini Iran iwapo tu Qatar haitoshambuliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *