Wadau Katika sekta ya usuluhishi nchini wamehimizwa kushirikiana na serikali katika kuongeza ushiriki wa wanawake katika utatuzi wa migogoro inayojitokeza katika jamii ambayo athari zake huwafikia watu wengi bila kujali jinsi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi (TIAC), Wakili Godson Nyange amesema watafanya kongamano la siku tatu la ‘Njia Mbadala za Utatuzi wa Migogoro (ADR)’ ili kuwawezesha wanawake kujenga uwezo, kujiamini pamoja na kuongeza ufanisi wao katika kushiriki kikamilifu kwenye mchakato wa utatuzi wa migogoro nje ya mahakama.

Mwandishi @esterbella_malisa

Mhariri | @moseskwindi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *