Kuelekea Sikukuu ya Eid Fitri, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) Mkoa wa Dodoma imetoa msaada kwa watoto yatima na wenye mahitaji maalumu katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Rahmani.
Kaimu Meneja wa TRA Dodoma, Obrey Sillayo amesema mamlaka hiyo itaendelea kushirikiana na taasisi na jamii katika shughuli za kijamii, huku akipongeza kituo cha Rahmani kwa malezi bora na maadili wanayowapa watoto.
Mratibu wa kituo hicho, Rukia Hamisi Abdallah ameishukuru TRA kwa msaada huo, akibainisha kuwa umeleta faraja na matumaini kwa watoto, huku pia ukionyesha mshikamano wa kijamii na uwajibikaji wa taasisi za umma katika kusaidia makundi yenye mahitaji maalumu.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)