#HABARI: Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imefanya ziara katika bandari kavu ya Kwala kwa lengo la kujionea utendaji kazi na kukagua maendeleo ya mradi huo.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo iliyofanyika Machi 19, 2026, Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema bandari kavu ya Kwala inaongeza ufanisi katika bandari ya Dar es Salaam kwa kupunguza msongamano, huku akieleza jitihada zinazofanyika kuhakikisha nchi mbalimbali zinapitisha mizigo katika bandari ya Dar es Salaam.
Miongoni mwa jitihada zinazofanyika ni pamoja na kuzipatia nchi hizo maeneo ya kuhifadhi mizigo ambapo katika bandari kavu ya Kwala nchi ya DRC imepewa eneo lenye ukubwa wa hekta 45, Zambia hekta 20, huku nchi za Burundi, Malawi, Rwanda, Sudan Kusini, Uganda na Zimbabwe zikikabidhiwa maeneo yenye ukubwa wa hekta 10 kila moja.
Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo Selemani Kakoso kwa niaba ya wajumbe, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji uliofanyika katika bandari hiyo, na kutoa kongole kwa Waziri Mbarawa kwa utendaji kazi katika sekta ya uchukuzi.
Aidha, ameongeza kuwa mradi huo ni mzuri huku akitoa wito kwa wananchi kuamini utendaji kazi wa serikali kwani wao kama wabunge kwa niaba ya watanzania, wamejionea na kuridhika.
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.