#HABARI: Kamati ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI imepitisha rasmi Randama ya Mpango na Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) kwa mwaka wa fedha 2026/27.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Florent Kyombo, ameeleza kuwa lengo kuu la bajeti hiyo ni kuwaletea tabasamu Watanzania kwa kuboresha huduma za msingi kote nchini.
Maelekezo ya kamati yameitaka wizara kuhakikisha utekelezaji wa bajeti hiyo unaleta tija katika sekta za afya ya msingi, elimu, na ujenzi wa miundombinu ya barabara kupitia TARURA.
Aidha, kamati imesisitiza umuhimu wa kuimarisha utawala bora ili huduma hizo ziendane na maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwatumikia wananchi kwa ufanisi.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi (TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe, amewashukuru wajumbe wa kamati na kuahidi kuwa ofisi yake itasimamia kikamilifu utekelezaji wa mpango huo.
Amesisitiza kuwa watumishi wote wamejipanga kuhakikisha rasilimali zilizotengwa zinatumika kuleta matokeo chanya na tabasamu la kudumu kwa wananchi mara baada ya bajeti hiyo kupitishwa na Bunge.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.