#HABARI: Timu ya waandishi wa habari kutoka ITV na Radio One ikiongozwa na Mkuu wa kitengo cha michezo Bwana Amri Masare, leo imemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu na kupokelewa vyema ofisini kwake.

Ziara hiyo imelenga maandalizi ya kazi za kihabari kuelekea tamasha la Kili Marathon linalotarajiwa kufanyika Machi 22, 2026 katika Manispaa ya Moshi.

Akizungumza wakati wa mapokezi hayo, mkuu wa mkoa amewakaribisha waandishi hao na kusisitiza umuhimu wa kuripoti habari kwa weledi ili kuendelea kuitangaza vyema Mkoa wa Kilimanjaro kupitia matukio ya michezo.

Tamasha hilo linatarajiwa kuvutia washiriki wengi kutoka ndani na nje ya nchi, likiwa ni miongoni mwa matukio makubwa ya michezo na utalii nchini.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *