Imebainika kuwa viboko vina mchango mdogo kwenye kukabiliana na utoro wa wananfunzi shuleni kuliko mazingira yenye mvuto kwa Watoto hao.

Tafiti mbalimbali zilizojikita kuangazia mazingira ya elimu ukiwemo wa Benki ya dunia mwaka 2019 pamoja na ripoti za HakiElimu na Uwezo zinapendekeza kuwa haihitaji nguvu kubwa ama mijeledi ili kumvutia mtoto Kwenda shule.
Ni kupitia michezo, walimu wenye upendo, miundombinu bora kama madarasa yenye yenye mvuto, na uwepo wa dawati za kutosha humvutia mtoto na kumpa motisha ya kuhudhuria shule na kupenda kusoma.

Kama sehemu ya kuhitimisha shamra shamra za maadhimisho ya siku ya wanawake duniani iliyofanyika mwezi huu,mfuko wa Serikali wa SELF MF ulio chini ya Wizara ya fedha wamewaongezea tabasamu watoto hawa kwa kuwakabidhi dawati 42 zenye uwezo wa kubeba zaidi ya wanafunzi 130
Akikabidhi msaada huo Mkurugenzi Mkuu wa SELF MF Bi Santiel Yona anasema wameguswa na uhitaji wa shule na kuvutiwa n jitihada za walimu.

Kwa Upande wa uongozi wa shule hiyo kupita mwalimu mkuu weke Godfrey Shubi pamoja na mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Robert Karia , Wanakubali kuwa suala lolote linaloboreshwa shuleni ni heshima kwao na deni la kuendelea kuwanoa Watoto walioaminiwa kuwasimamia

Mfuko wa SELF kama wadau muhimu katika shule hii ya msingi Mikocheni inakuwa mfano kwa wadau wengine kumulika changamoto zinazowafanya Watoto wasipende shule. Mazingira bora na elimu bora vinatoshana nguvu kuwafanya Watoto wasiburuzwe kuwapo shuleni bali wapende wao wenyewe kwa kuona vitu vizuri kwenye mazingira ya kujifunzia.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *